Tuesday, February 14, 2017

MRADI WA UFUGAJI SUNGURA

Image result for MRADI WA UFUGAJI SUNGURA

KIBANDA CHA KUFUGIATunasaidia kwenye ujenzi wa vibanda bora vya sungura,  kwagharama ya Tshs 65,000/=  tu    kwa kimoja cha  ukubwa  wa  futi 2.53  ,  chenye  uwezo  wa  kufugia  Sungura  mmoja  mkubwa  wakuzalisha  pamoja  na watoto wake kwa mwezi mmoja baada yakuzaliwa yaani kipindi chote cha unyonyeshwaji, na kibanda cha saizi hiyo pia kinaweza kufugia hadi sungura kumi wa umri wa miezi mitatu.
Tunashauri ujenzi wa vibanda vitatu kwa kila jike (kupata nafasi ya watoto wanaomaliza kunyonya kwani jike huzaa kila baada ya miezi 2) na pia kibanda kimoja kwa kila dume.

MBEGUTunawataka wakulima wetu kufuga mbegu bora na halisi ya sungura watakaotupa nyama bora kwa soko letu,  na  tunawauzia  kwa  gharama  ya  Tshs  80,000/=  kwa  kila  jike  aliyetayari  kubeba  mimba   na  Tshs 40,000/= kwa kila dume mwenye umri wakuzalisha.

MAFUNZO YETUTuna  mafunzo  mara  kwa  mara  pia,  na  zaidi  kuhusu  ujezi wa  mabanda  bora,  Utunzaji  na  ufugaji  kwa ujumla, na kuhusiana na maswala ya magonjwa na namna yakuzuia.Tuna  saini  mkataba na mkulima/mfugaji  (kwa  ada  maalum  kila  mwaka)  ambao utamuhakikishia mfugaji/mkulima  soko kwa kipindi chote cha mkataba  pale sungura wake wanapokuwa tayari kwa kuuzwa.Tunanunua sungura katika umri wa miezi 4-5. Kwa umri huo sungura mwenye afya aliyelishwa vizuri anapaswa kuwa na uzito wa kilo 3-4, na kilo moja ya sungura akiwa hai tunamnunua kwa Tshs8,000/=.

Tafadhali zingatia mafunzo kwa mtunzaji wa sungura wako/au kama ni wewe mwenyewe ni ya muhimu kujifunza mambo ya msingi unapoanza mradi nasi,Paleunapohitaji ushauri wa kitaalam utagharimia nauli ya mtaalamu atakufundisha UFUGAJI BORA WAKISASA kwa vitendo.

Related Posts:

  • CHAKULA CHA NGURUWE NA ULISHAJI Chakula bora kwa Nguruwe ni moja  ya suala muhimu sana kwenye dhana nzima ya ufugaji wa Nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha Nguruwe kinagharimu kama asilimia sabini ya garama zote za ufugaji wa ngur… Read More
  • MATUNZO YA WATOTO WA NGURUWE Kwa kawaida hunyonya kwa wiki 5 -8, na baada ya hapo hutengwa na mama yao na kuanza kupewa chakula chenye protini 30% kwa muda wa wiki 6 za mwanzoKUKATA MENOMara baada ya kuzaliwa watoto wakatwe meno kwa kutumia mkasi mkubwa… Read More
  • CHANJO ZA KUKU - RATIBA MAALUM      SIKU 1.   Baada ya vifaranga kutotoleshwa ndani ya siku moja wapewe glucose kwa muda wa masaa mawili. Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa na baada ya hapo vifaranga wap… Read More
  • MAGONJWA MAKUU YA NDEGE Magonjwa huainishwa kulingana na baiolojia yao,kama Virusi,Bakteria,Kupe,ukungu,na chanzo chao,kwa mfano magonjwa ya lishe yaliyoangaliwa hapo juu.Hata hivyo,magonjwa makuu katika ndege yamegawanywa katika makundi mata… Read More
  • DONDOO ZA ZIADA KATIKA UFUGAJI WA KUKU VITU AMBAVYO HUTAKIWI KURUHUSU KUKU WAKO WALE. Kuna baadhi ya vitu uwa tunawapa kuku kwa mazoea au tunawaachia tu tunapoona wanakula lakini ukweli vinakuwa na madhara hebu tuviangalie; VITUNGUU vitunguu… Read More

0 comments:

Post a Comment