Tuesday, February 14, 2017

UFUGAJI WA KUKU WENYE TIJA

Image result for kuku wa kienyeji
Wengi wetu tunafuga kuku pasi na malengo, nimekaa chini na nikaona uchoyo ni jambo moja baya sana linalotuumiza sana watanzania katika maendeleo ya kila jambo. (Hasa uchoyo wa mawazo, tunalaumu mno hatutoi mawazo yenye tija)Leo naongelea kuhusu ufugaji wa kuku, hasa kuku wa kienyeji ufugaji wenye tija.
Kuku hawa ni rahisi sana kuwafuga lakini ni wagumu sana kama hutokuwa makini na kama huna malengo na ufugaji wako.  Wengi wetu tunafuga tu huku tukiwa na matarajio makubwa ya mafanikio.  Unajidanganya ndugu yangu, huwezi kutegemea kitu ambacho hukipendi na hukigharamii.  Kuku wanatakiwa kula, kuku wanatakiwa kunywa, kuku wanatakiwa kupata huduma za dawa, kuku wanataka kulala sehemu nzuri na safi, yenye hewa, wanapopendwa, wanapojaliwa, kuku wanahisia kama viumbe wengine huwa wanapenda wakiwa na shida uwaangalie kama unavyoangalia kitu kingine chenye uhai na uwasaidie, lakini ukiwa mkaidi kwao nao watakuletea ukaidi.  Haya ni maneno huwa naambiwa na mama yangu mzazi bi Paulina, huwa anawaangalia kuku wangu na anasema hawa kuku wana shida lakini huwaelewi, sasa nimeanza kumuelewa na ndio maana nataka nikupe elimu hii nawe uweze kufaidika.

ONDOA UCHOYO KWANZA

Kama umeamua kufuga kweli basi fanya haya, usiwe bahili wa muda kwa kuku wako, usiwe bahili wa vitu vifuatavyo;
a.       Fedha za kununulia chakula
b.      Fedha za dawa na daktari
c.       Fedha kwaajili ya kununua mboga za majani au ufanye kilimo cha mboga za majani ili uwalishe
d.      Fedha kwaajili ya ulinzi wa kuku wako
e.       Fedha kwa mtunzaji wa kuku wako
f.       Fedha za usafirishaji kwenda kwa wateja wako, au katika manunuzi ya kuku wageni

Image result for kuku wa kienyejiImage result for kuku wa kienyeji

Lakini kuna jambo kubwa zaidi, umoja kati yako wewe na wafugaji wenzako.
Na hii leo ndio mada yangu kuu.
Umoja wa wafugaji katika eneo hilo ulilopo, ndio nguzo kuu ya kupata kipato kikubwa zaidi na kuwa na soko kubwa zaidi mwaka mzima na miaka yote na hakuna mtu anatakayekosa huduma ya kuuziwa kuku au mayai katika eneo lenu ikiwa mtakuwa wamoja kwa ufugaji wa kuku.

LENGO MOJA NA MOYO MMOJA
Ni vigumu sana kwa watu zaidi ya 100 kuwa na lengo moja kwa miaka zaidi ya 10, lakini kama mtaamua na mkaona faida yake inawezekana tena kwa 100%.  Naongea haya kwa kuwa naona kabisa ili ufanikiwe kuwa kama unataka kuku 10,000 kwa kipindi kifupi ni ngumu lakini wafugaji 30 mkiunda kikundi na mkachangishana labda shilingi 500,000 kwa kila mmoja mtapata shilingi za kitanzania 15,000,000.  Mkiamua sasa mjenge banda la shilingi 3,000,000 zitabaki 12,000,000. Na mkinunua chakula cha shilingi 3,000,000 zitabaki milioni 9,000,000.  Wengi wa wauzaji wa kuku huuza kuku waliochanjwa hivyo unaweza kukaa na kuku wale kwa miezi mitatu zaidi wakiwa wako vizuri bila kuugua. Nunueni kuku kwa shilingi 1,600, leo nakupa siri kama ulikuwa hujui nipigie simu nitakuambia vizuri wapi pa kununulia na utashangaa utakuja kuwa na kuku hadi ulie. Katika milioni 9,000,000 zilizobaki nunua kuku wa shilingi 5,000,000 kwa kila mmoja kumnunua kwa shilingi 1,600 utapata kuku wangapi? 
Utapata kuku 3,125.  Kuku hawa utawanunua wakiwa na umri wa miezi mitatu na nusu, hivyo utawakuza kwa miezi miwili na nusu wataanza kutaga.  Lakini kama mtataka kuwa na kuku wengi zaidi kwa muda wa miezi 6 mnaweza kuwa kundi lenu la watu 30 mkawa mnachangishana 200,000 kila mmoja ina maana kila mwezi mtapata shilingi 6,000,000 x 6 = 36,000,000.
36,000,000/1,600 = 22,500
Kundi litapata kuku 22,500 ina maana kama kuku mmoja baada ya miezi minne atauza kwa shilingi 10,000 kwa kuku 22,500 kikundi kitapata shilingi 225,000,000.
Kwa maana hii kikundi kitakuwa kimepata faida ya shilingi;
225,000,000 – 36,000,000 = 224,964,000
224,964,000 – 50,000,000 = 174,964,000
Hiyo hesabu ni makadirio na matumizi ya kilichopatikana ilitumika 36,000,000 kununua kuku 22,500 wakauzwa kwa shilingi 10,000 kwa kila mmoja ikapatikana shilingi 225,000,000 tunatoa fedha ya manunuzi iliyokuwa shilingi 36,000,000 hivyo itabaki shilingi 224,964,000 katika pato hilo la 224,964,000 toa 50,000,000 ya vyakula, maji, mlinzi, mhudumu, umeme na maji utabaki na shilingi 174,964,000 (weka hasara ya kuku wengine kufa) faida itakuwa 100,000,000
Image result for kuku wa kienyejiImage result for kuku wa kienyeji

Hii inaweza kufanya kila mwanachama wa kikundi akawa na faida ya shilingi 3,333,333.30 ambapo mkiamua kujiwekea malengo ya kuuza kuku kwa mizunguko 1,000 kila mwanakikundi atakuwa na faida ya shilingi 333,333,300 na hii inawezekana sana kama kundi lina nia na linaupeo na si kulalamika kila wakati.  Tatizo letu watanzania ni walalamishi sana sio wote ila asilimia kubwa ni walalamishi.  Nina hakika kundi hili linaweza kujikwamua kwa kuku tu bila kujichanganya na jambo lingine.  Kundi likijipa miaka mitano ya kufanya biashara hii kwa nguvu na nia itakuwa mfano wa kuigwa.
Kumbuka kuna kundi la kwanza la kuku 3,125 ambapo kuna shilingi 4,000,000 ilibaki benki kama kilinda benki, kikundi hiki kwa mahesabu yale yale kina uwezo wa kutengeneza shilingi  na shilingi za mamilioni.  Ila sasa huku itazitengeneza kwa kuzalisha mayai ya kuku wa kienyeji.

MAYAI YA KIENYEJI
Ikiwa kuku  3,125 majogoo yatakuwa 1,125 na majike 2,000 basi una uhakika wa kuwa na trei 66 kwa siku.  Chukulia mfano siku 7 za wiki unachukua mayai manne tu kwa wiki utapata mayai 16 kwa kuku hii inamaana utapata mayai 32,000 kwa mwezi ambayo ni trei 1,066.  Trei moja ya mayai ikiuzwa shilingi 12,000.
1,066 x 12,000 = 12,792,000 kwa mwezi
12,792,000 x 12 = 153,504,000 kwa mwaka
Image result for MAYAI YA KIENYEJI
Kwa maana hiyo mayai yanaweza kuingiza shilingi 153,504,000 ukitoa gharama za usafirishaji na mhudumu mnaweza ingiza 100,000,000 kwa kuuza mayai ya kienyeji pekee.
Kwanini tusijiunge tukafanya shughuli hii?
Unasubiri nini?
Unataka kuona nimetajirika kwanza ndio na wewe uhamasike?
Usiwe mchoyo njoo tujiunge tukuze kipato kwa biashara hii niliyokupa sasa hivi

MBOLEA  YA KUKU
Kinyesi cha kuku ni mbolea nzuri sana kwa wakulima, kwa idadi ya kuku iliyopo katika kikundi na inayoendelea kuwepo kila mfuko wa mbolea ya kuku inauzwa shilingi 2,000.  Ikiwa kikundi kitakuwa na mifuko isiyopungua 2,000 basi kikundi hakitakosa shilingi 4,000,000 iliyotokana na mbolea.

Image result for UFUGAJI WA KUKU


0 comments:

Post a Comment