Tuesday, February 14, 2017

Mambo Ya kuzingatiaKatika utunzaji wa vifaranga

Image result for Mambo Ya kuzingatiaKatika utunzaji wa vifaranga
ufugaji wa kuku imekuwa ni kazi muhimu na inayokubalika katika jamii nyingi. Ni kazi isiyohitaji gharama kubwa sana, ambayo imekuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa kwa wanaiofanya kibiashara. 

Tatizo ambalo limekuwa sugu na kusababisha hasara kwa wafugaji walio wengi, ni kutofahamu namna bora ya kuwatunza vifaranga kuanzia siku ya kwanza wanapoanguliwa hadi kuwa kuku wakubwa. Hali hii imekuwa ikiwasababishia wafugaji hasara na kuwakatisha tamaa.
Hii inatokana na wafugaji kuzingatia kuwa na banda na chakula tu, bila kuzingatia aina nyingine ya matunzo muhimu yanayohitajika kwa ajili ya kuwafanya vifaranga waishi na kukua wakiwa na afya.
Haya ni baadhi ya mambo muhimu kuanzia siku ya kwanza ili vifaranga wako wasipate madhara na hatimaye kufa: Mara baada ya kuanguliwa, vifaranga wawekwe sehemu yenye joto kwa wastani unaohitajika.• Hakikisha sehemu ya banda ulipowaweka vifaranga ni kavu, na isiyokuwa na vimelea.• Hakikisha vifaranga wote wanapata chanjo ya mahepe (mareks) siku ya kwanza.• Siku ya saba, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa kideri.• Inapofika siku ya 14, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa gumboro.• Rudia chanjo ya kideri katika siku ya ishirini na moja.• Siku ya ishirini na nane, rudia tena chanjo ya gumboro• Baada ya wiki nane, hakikisha kuwa vifaranga wako wanapata chanjo ya ndui.Kwa kuzingatia mtiririko huo, utakuwa na uhakika kuwa kuku wako ni salama. Watakuwa bila tatizo, jambo ambalo litakupa uhakika wa kuwa na mazao bora, na hatimaye kupata faida.Pamoja na hayo, hakikisha kuwa unazingatia lishe bora. Hii itasaidia kuwapa kuku afya njema na kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa.
**Kamwe usiwape kuku vyakula vilivyooza. Hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa kuku na kusababishia hasara.

Related Posts:

  • MAGONJWA YA KUKU, DALILI, KINGA NA TIBA Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa… Read More
  • Mashine za kutotolea Vifaranga Pata vifaranga vya kuku wa kienyeji aina sasso kwa bei poa na kwa Mkopo.Kifaranga sasso 1@1500cashMkopo ni miezi 3..Kifaranga sasso kwa mkopo 1@1650.Vifaranga vya kuanzia cku moja na kuendelea. Kwa maelezo zaidi piga 071… Read More
  • UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI NA MAFANIKIO YAKE Kama ilivyo chunvi ya dunia, ufugaji pia huhitaji upendo, uvumilivu, karama, utu na maombi ya dhati ambayo yatazaa namna nzuri ya kuipenda kwa dhati ya moyo wako kazi hii ya ufugaji. Vinginevyo utabakia kuwa mtu wa kujarib… Read More
  • FURSA MBALIMBALI ZA BIASHARA NA MIRADI Changamkia Fursa mbalimbali ujikwamue Kimaisha Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha. Kutengeneza na kuuza tofali Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmash… Read More
  • UFUGAJI WA SAMAKI Nyanja ya ufugaji wa samaki inajumuisha ukuzaji wa viumbe vya kwenye maji (bahari na maji baridi) katika mazingira tofauti na yale ya asili. Lengo kuu ni kukuza kwa muda mfupi ili kujipatia lishe, kipato na kutunza mazi… Read More

0 comments:

Post a Comment