Monday, March 6, 2017

KILIMO CHA VITUNGUU SAUMU (Garlic)

Image result for KILIMO CHA KITUNGUU SAUMU


UDONGO
Vitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si ya kutosha kwenye udongo, tumia samadi iliyokwisha oza vizuri usitoe samadi bandani na kuipeleka shambani moja kwa moja kwenye shamba la vitunguu thwaumu, labda kama utaliacha shamba bila kulimwa kwa zaidi ya miezi 6, pia unaweza kutumia mbolea za viwandani kama ammonium nitrate, ammonium sulphate, urea n.k wakati wa kupanda na kila baada ya wiki 4 – 6 mara mbili zaidi

UPANDAJI 
Image result for UPANDAJI WA KITUNGUU SAUMU
Kipindi kizuri kwa upandaji ni kipindi ambacho hakuna joto hasa miezi ya May mpaka August kwa Tanzania, Unachukua kitunguu twaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 10 na kati ya mistari ni sentimeta 30. Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kungolewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu thwaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu.
Image result for UPANDAJI WA KITUNGUU SAUMU

UMWAGILIAJI

Kama kuna upungufu wa mvua au ni kipindi cha kiangazi basi ni vizuri ukamwagilia shamba lako, wakati mzuri wa kumwagilia vitunguu twaumu ni asubuhi na sio jioni au mchana, hii inasaidia vitunguu twaumu kujijengea uwezo wa kupambana na magonjwa, baada ya mizi miwili unaweza kupunguza umwagiliajai huku ukiangalia kwa kuchimba kidogo kama vitunguu twaumu vimezaliana vya kutosha na kuanza kukomaa, ukiona vimekomaa acha kabisa kumwagilia ili visioze

UANGALIZI
Aina nyingi za vitunguu twaumu vitakuwa kama vinatoa mbegu kwenye mmea (angalia picha chini), ingawa kuna nadharia nyingi lakini inashauriwa kukata hizi mbegu chini kabisa kwa kisu kikali na kisafi, usikate mapema mara baada ya kutokeza bali subiri mpaka mmea unapoanza kama kujikunja ndipo ukate, kwa wale wanaoacha mbegu hizi ukiamua kuzipanda kwa msimu wa kwanza zitazaa kitunguu kimoja tu cha duara lakini chenyewe ukikipanda tena kwenye mzunguko wa pili kitazaa vitunguu vingi kama kawaida



Ungoleaji wa magugu na majani ni muhimu muda wote ili kuondoa kugombea rutuba, hewa na maji shambani, kwa wenye mashamba makubwa wanaweza kutumia dawa za kemikali kama ROUNDUP na nyinginezo ili kudhibiti magugu, ingawa mimi sishauri hivyo.

MAGONJWA
Magonjwa kama botrytis (kuoza shingo) blue mould na fusarium (kuoza kwa vitunguu) husababisha hasara kubwa kama hayatadhibitiwa kwa kutumia viuatilifu mara unapoona dalili, pia magonjwa kama white rot huchukua zaidi ya miaka 20 kuondoka kama yatavamia shamba lako, inashauriwa kufanya mabadiliko ya zao kila baada ya miaka mitano kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii moja kama vitunguu maji, unaweza kupanda maharage, mahindi, karoti na kabichi katika mzunguko huo. Pia magonjwa kama kutu ya majani husababisha na unyevu mwingi hasa kama mimea itakuwa kwenye udongo unaotuamisha maji au mimea kumwagiliwa jioni au usiku, kumbuka kumwagilia asubuhi tu Ili kudhibiti ugonjwa huu wa kutu mimea ingolewe na ichomwe au utumie viuatilifu vya kuulia fangasi wa mimea.

Related Posts:

  • KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO Jina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha. Kilimo hiki … Read More
  • KILIMO CHA MATIKITI MAJI Ili kulima matikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na ardhi yenye rutuba ya kutosha, matikiti maji hukua haraka kama mimea mimgine ya jamii yake itambaayo mfano Matango, maboga n… Read More
  • KILIMO BORA CHA MINAZI UPANDAJIUko wa ina mbili kuna wa vibox na wa pembetatu lakini kwa aina zote mbili umbali wa kupanda ni mita 7.6 kutoka shimo hadi shimo la mnazi, kiasi cha mashimo 175 kwa hecta huingia na kama utatumia mtindo wa pembetatu… Read More
  • MAGONJWA MAKUU YA NDEGE Magonjwa huainishwa kulingana na baiolojia yao,kama Virusi,Bakteria,Kupe,ukungu,na chanzo chao,kwa mfano magonjwa ya lishe yaliyoangaliwa hapo juu.Hata hivyo,magonjwa makuu katika ndege yamegawanywa katika makundi mata… Read More
  • KILIMO CHA VITUNGUU SAUMU (Garlic) UDONGOVitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si ya kutosha kwenye udongo, tumia samadi iliyokwisha oza vizuri usito… Read More

0 comments:

Post a Comment