Tuesday, February 14, 2017

Mafunzo ya Ufugaji wa kuku Kitaalamu

Image result for ufugaji wa kuku
Wanagroup karibuni tena tujifunze
Kwanza nawashukurun sana wale tunaotiana moyo.Ahsateni sana.
Nipende kuwaulizeni wale mnaokuja inbox nakutoa maneno ya kejeli nayakudhihaki mnafikiei maneno yenu yatanikatisha tamaa??
Nawaomben sana kama unania nakujifunza njoo kwa lengo zuri maneno machafu hayana nafasi pamoja na zihaka zenu
Nawaombeni mjiunge magroup ya vunja mbavu uislam na ukristo
Huko ndo mkatoe maneno yenu yasiyo na maana
Kwa wale tunao enda sambamba nisamehen kwa kuanza na maneno haya
TUENDELEE
Leo nivyema tukaangalia Magonjwa yanayo shambulia kuku Mara kwa Mara pamoja na vidusia vya ndani na nje
Kwakuwa magonjwa mengi hayana tiba.
Inatakiwa kinga kufuatiliwa na kutolewa katika muda muafaka.
Maada hii itaelezea kwa ufupi aina ya magonjwa jinsi yanavyo ambukizwa
Dalili
Kinga. Na
Tiba
Kadhalika vidusia wa ndani na nje wanaoshambulia kuku wataelezwa
Baadhi ya magonjwa hatari ya shambulio kuk(ndege)
Kideri/New Castle/mdondo
Ndu/fowl pox
Kipindupindu/fowl cholera
Mafua ya kuku /Infectious Coryza
Homa ya matumbo/fowl Typhoid
Kuhara damu /Coccidiosis
Ukosefu wa vitamin A
Leo tuanze na kideri
KIDERI/New castle
Uginjwa huu huwapata kuku rika zote wakubwa kwa wadogo.
Nimiongoni mwa magonjwa hatari ambayo huambukizwa kwa kasi kubwa sana na kusababisha vifo.
Ugonjwa huu husababishwa na virus na huweza kushambulia pia Bata,Bata mzinga,kanga,kwale, nk
Jinsi unavyoambukiza
**Kuku kuvuta hewa yenye virus vya ugonjwa huu toka kwa kuku mgonjwa
** upepo huweza kuhamisha virus vya ugonjwa huu toka sehemu hadi sehemu nyingine
**watu huweza kuhamisha ugonjwa huu wanapotembea toka sehemu hadi sehem.kula nyama ya kuku aliyekufa kwa ugonjwa huu na kujisaidia ovyo haja kubwa na ndogo
**kuku wasio wagonjwa na kukaa na kuku wagonjwa
**Ndege wanaokula mizoga kama kunguru huweza kusambaza mabaki ya mizoga yenye ugonjwa
**vyombo vya usafri kutoka eneo lenye ugonjwa
Dalili zake
Homa kali,kuku kuwa dhaifu,kuzubaa na kushusha mabawa na kupoteza hamu ya kula
Kuku kupoteza fahamu nakupooza viungo
Kulegea kwa shingo na inaweza kupinda na kuelekea nyuma au pembeni.pia huweza kuzungusha shingo
Kuhema kwa shida na hutoa majimaji mdomoni yenye harufu Kali
Kukuhoa,kukoroma,na kupiga chafya
Kuharisha kinyesi chenye rangi ya kijani
Vifo mfululizo vinaweza kumaliza kuku wote bandani Nk
Matibabu ya kideri
Ugonjwa huu unaambukizwa na virus hivyo basi hauna tiba bali kinga
MUHIMU
Usichanje kuku kama ugonjwa umeshaingia kwenye kundi
Kuna aina mbili za chanjo
A@:chanjo inayoweza kuvumila joto{Thermostable}
Chanjo hii inaweza kutunzwa ktk hali ya joto la kawaida (room temperature)na kuendelea kubaki salama kwa muda wa siku 30.
Hutolewa kwa nji ya matone kwenye macho
Kwakutumia chanjo hii unaweza ukawachanja kuku kwa muda wowote kila siku.
Ila inashauriwa kuwa chanja Asubuhi ili kupunguza uwezekano wa chanjo kupata miare ya jua ya moj kwa moja.
MUHIMU
Inashauriwa kuweka chanjo hii chini ya chombo kinacho wekamtungi wa maji kama hauna friji.
Hii huongeza zaidi usalama wa chanjo hii.
Pia si vye.a kubeba chanjo hii kwenhe karatasi za plastiki kwani hizi huweza kuongeza joto zaidi.
B@:chanjo isiyo vumilia joto
Chanjo hii hutunzwa kwenye ubarid i muda wote .hutolewa kwa kuku kwa kuchanganya na maji ya kunywa kuku.
Ikisha changanywa huchukua mda mfupi kama saa moja na baa ya hapo inaanza kupoteza ubora wake
Kwa hali hiyo inashauliwa kuwanyima kuku maji kwa muda ili wapate kiu haswa na ndipo uwawekee maji ya kunywa yenye chanjo ili wanywe kwa wingi nakwamda mfupi.
Pia inashauriwa siku ya chanjo wape kuku chakula kikavu zaidi kabla ili wapate kiu sana.
MUHIMU
Kideri ni ugonjwa tishio ambao huweza kumaliza kuku wote kundini au mtaa mzima!!!!!
Kideri kikitokea vifo huwa vingi
Kideri huweza kuzuiwa kwa kinga kila baaaada ya miezi mitatu
Wafugaji wa kuku waunde vikundi vya ushirika vya kuchanja kideri.
********MWISHO**********
Panapo majaliwa kesho tutaendelea
Kuna watu wanahitaji namba zangu
Lkn hawa watu wasumbufu ndo wananipa shida.
Lajin nitazitoa kesho
KARIBUNI. Kwa....
Ushauri
Maswali
Nyongeza nk
NB:midahalo na mabishano hayana nafasi we kama hujui kitu kaa kimya usije ukatia watu hasara bure
Ahsanten

0 comments:

Post a Comment