Monday, March 6, 2017

MATUNZO YA WATOTO WA NGURUWE

Image result for WATOTO WA NGURUWE
Kwa kawaida hunyonya kwa wiki 5 -8, na baada ya hapo hutengwa na mama yao na kuanza kupewa chakula chenye protini 30% kwa muda wa wiki 6 za mwanzo

KUKATA MENO
Mara baada ya kuzaliwa watoto wakatwe meno kwa kutumia mkasi mkubwa au kifaa cha kukatia waya (wire cutter) umuhimu wa zoezi hili ni kwa sababu nguruwe huzaliwa na meno na mara wanapoanza kunyonya huumiza chuchu za mama yao na kumsababishia ugonjwa wa chuchu (mastitis)

KUHASI
Madume ambayo yatakuzwa kwa ajili ya nyama ni vizuri yakahasiwa, hii husaidia ukuaji wa haraka na pia huondoa harufu ya balehe, Zoezi hili lifanyike wakati wakiwa na wiki 3 inapofika wiki ya 5 zoezi huanza kuwa gumu kwa sababu watoto wanakuwa wakubwa na litahitaji sindano za ganzi, zoezi hili linahitaji mtaalamu wa mifugo.

MINYOO
Mzazi anapokaribia kujifungua wiki ya mwisho achomwe sindano ya kuondoa minyoo na magonjwa ya ngozi ijulikanayo kama IVOMEC SUPER au IVERMECTIN zinazopatikana kote nchini, dawa hii husaidia kuwalinda watoto na minyoo hadi wanapoacha kunyonya ndio na wao wapigwe sindano hii ambayo pia itasaidia kuua minyoo ya mapafu, minyoo ya macho, viroboto na kuondoa ukurutu.

CHAKULA
Baada ya wili chache vitoto vitaanza kula chakula kidogo kidogo kwa kuanzia na kile anachopewa mzazi, hakikisha mzazi anapewa chakula kingi na chakutosha kwa sababu atakuwa anakula yeye na watoto wake

0 comments:

Post a Comment