Thursday, February 16, 2017

UTAJIRI KATIKA MIRADI YA KUFUGA KUKU

Image result for mafanikio katika ufugaji wa kuku

Mradi wa kufuga kuku ni mradi ambao huleta faida kwa muda mfupi sana.
Ili upate faida kubwa ni vizuri ukawa na mradi ambao unaweza kuumudu kwa kuwa na mahitaji muhimu katika mradi wako.

MFANO, mtu anayetaka kufuga kuku tuseme 500 anatakiwa kuwa na vifaranga 550. Awe ana uwezo wa kuwalisha hao vifaranga na kuwapa tiba. Pia awe na uwezo wa kujenga banda bora.
Image result for mafanikio katika ufugaji wa kuku
 Baada ya hapo kinachotakiwa ni umakini wa kufuatilia mradi katika kipengele cha utoaji huduma kwa kuku hao. Katika kundi hilo la kuku 500, 50 wanatakiwa kuwa majogoo na 450 mitetea.
Katika hao mitetea 450 aslimia 75 wanatakiwa watage kila siku. Asilimia 75 ya 450 ni kuku 337.

Mayai ya kuku hawa huuzwa kwa Tsh. 300@. Hivyo kila siku utapata Tsh 337 x 300 = Tsh. 100000.

Kama mtu anaweza kupata Tsh. 100000 kila siku kwa mwezi una uhakika angalau wa kuweka akiba ya Tsh. 100000 bila shida. Kama utaweka akiba ya fedha hiyo kila mwezi bila shida kwa mwaka utakuwa umeweka akiba ya shilingi milioni kumi na mbili.

Watu wengi wanaweza kufikiri hii ni nadharia ambayo haiwezekani, UKweli ni kuwa hiki kitu kinawezekana bila shida kabisa.

Ikiwa utahitahiji usaidizi njoo kwetu tukuelekeze namna unavyoweza kuondokana na umaskini usio wa lazima.

Kumbukeni ndugu wajasiriamali kwamba ukiamua ni kweli ndoto yako itatimia.
UENDESHAJI WA MRADI WA KUKU

        Image result for mafanikio katika ufugaji wa kuku

UENDESHAJI WA MRADI WA KUKU WA MAYAI:

Iili kufanikiwa kufikia malengo ya kufuga kuku wa mayai  ni vyema mfugaji akapata wasaa wa kujiuliza maswali kadhaa ili awe na dira sahihi ya kile anachotarajia kufanya kutokana na mapato ya mradi huo.
Dira ni picha ya matokeo yanayotarajiwa yanayotokana na juhudi na maarifa .
Bila shaka kabla ya kuanza kufuga utakuwa umejiuliza ni kwa nini ufuge kuku wa mayai na wala sio kufanya kitu kingine ; swali kama hili litakusaidia kuwa na muelekeo wa kile unachotarajia na hivyo kuweka mkakati sahihi wa kusimamia mradi wako wa kuku wa mayai.Mfano , pengine umeamua kufuga kuku kwasababu kuna upatikanaji wa pembejeo kwa urahisi kama vile upatikanaji wa vifaranga, viinilishe, madawa na kubwa zaidi ni upatikanaji wa soko la mazao yako.
Vyovyote iwavyo mambo yafuatayo ni vizuri yakazingatiwa ili kupata mafanikio katika mradi wa kufuga kuku wa mayai;
1.      Uwe na uhakika wa kupata vifaranga kutoka kwa wasambazaji mahiri     ( reliable Day old Chicks breeders and Suppliers)
2.      Zingatia ratiba ya kulisha. Lisha kuku  chakula kinachopendekezwa kwa kuzingatia umri  na uzito.
3.      kagua na na fanya usafi mara kwa mara na katika nyakati zilizopangwa(inspect and carry out specificl and periodical hygienic operations)
4.      toa matunzo kwa kwa kuzingatia mahitaji ya makundi.
 
5.      Tengeza viota ili kuku waweze kutaga mayai kwa faragha bila bughudha kutoka kwa wengine. Vilevile viota husaidia kuwa na mayai safi na husaidia kuepuka kuvunja kuvunjika na kuchafuka kwa mayai mara kwa mara.
6.      Hakikisha unasafisha mayai kwa kitambaa safi  baada ya kuokota na kabla kuwauzia wateja.
7.      Zingatia matakwa ya wateja kwa kuainisha mayai katika makundi kama ifuatavyo;
  • Rangi ya mayai
  • Rangi ya kiini cha yai(egg yolk colour), wengi wanapenda kiini cha rangi ya njano.
  • Ukubwa wa mayai
  • Aina ya mayai( mayai ya kienyeji yanapendwa zaidi kuliko ya kisasa)
8.      Fanya ukaguzi wa afya za kuku na kuwa tibu kila mara. Utaratibu unaopendekezwa ni kukagua afya asubuhi unapoamka na usiku unapoenda kulala. Angalia vinyeo ili kuona wanakunya kinyesi cha rangi gani(kinyesi ni kielelezo muhimu katika kutambua ugonjwa).
9.      Chunguza tabia za kuku ili kuona kama wanakula mayai au la . Ukiona kuku wameanza kula mayai fanya zoezi la kukata midomo mara moja kazi hufanywa na wataalamu , kwahiyo unashauriwa kumuona mtaalmu aliye jirani.
10.  Tunza kumbukumbu zote mradi  ili zikusaidie kufanya tathmini ya mradi unaoendesha.

KULEA VIFARANGA VYA KUKU

Image result for mafanikio katika ufugaji wa kuku

Kulea Vifaranga kwa njia ya asili

Kuku aliyetotoa vifaranga anaweza kuachiwa avilee, lakini ili kuepuka majanga kama vile vicheche na mwewe inashauriwa watunzwe ndani ya uzio utakaowazuia ndege hao hatari kuingia na kuwachukua.
Kulea vifaranga kwa kutumia tetea ni njia ya asili itumikayo kuatamia, kuangua, kutotoa na hatimaye kuvilea hadi hapo wanapoanza kujitafutia chakula na kujihami dhidi ya maadui.
 Ili kutumia njia hii katika kuangua mayai kukutolesha mayai na kulea vifaranga ni lazima upate kuku mwenye tabia ya kuatamia (broody hen).
Kiota cha kuku anayeatamia hutengwa kutoka kwenye viota vya kutagia. Viota hivi huwekwa matundu mawili ya kuingiza hewa safi na kutoa ile chafu. Ukubwa wa matundu hayo ni inchi mbili za upana na urefu.
Andaa marandio mapya na kuweka mayai ya kuangua juu yake; chukua mayai ya kutosha kwenye kiota lakini yasizidi yale anayoweza kulalia  au kuyaatamia (kiasi cha mayai kumi na moja yanatosha kwa tetea mmoja).
Weka kiota sehemu isiyo na usumbufu kutoka kwa kuku wengine.kuku wanaofugwa katika kundi ni vizuri ukaweka kwenye uzio kwa wiki chache ili vifaranga wapate kuota manyoya.

Image result for mafanikio katika ufugaji wa kuku
Kuku aliyetotoa karibuni akiwafundisha vifaranga wake wadogo jinsi ya kula.

KULEA VIFARANGA WA UMRI  KUTOKA SIKU 1 HADI WIKI YA 4 KWA NJIA YA KISASA;

Mahitaji;
1.      Nyumba na vifaa
2.      Chakula
3.      Tiba ya magonjwa

MAANDALIZI YA NYUMBA/BANDA LA KULELEA  WIKI MOJA KABLA YA KULETWA VIFARANGA;
1.      Nyumba ya kulelea vifaranga ni lazima ifanyiwe usafi wiki moja kabla ya kuingiza vifaranga.
2.      Baada ya kupigwa deki au kufagiliwa itawekwa dawa ya kunyunyiza na   bomba [sprayer] sakafuni ukutani na upande wa ndani wa paa la nyumba. Dawa hii itasaidia kuua utitiri, chawa, viroboto na vimelea vya magonjwa mbalimbali. Dawa itatumika kadri ya maelezo ya watengenezaji.
3.      Baada ya kuwekwa dawa liache banda likauke kwa wiki moja kabla ya kuingiza vifaranga.
1.      KUTENGENEZA KIFAA CHA KULELEA VIFARANGA (BROODER AND HOOVER;
Image result for (BROODER AND HOOVER;Image result for (BROODER AND HOOVER;
Hiki ni kifaa maalumu cha kulelea vifaranga wasiotunzwa na mama yao.
Vifaa vya kutengenezea kifaa cha kulelea vifaranga
o   Ceiling board na au maboksi magumu
o   Wavu /kizuizi cha joto kali
o   Chanzo cha joto [jiko la mkaana mkaa, balbu –infra-red bulb]
o   Takataka za mbao /mabaki ya mpunga
o   Magazeti, / boksi laini
o   Mfuniko [hoover].
Kuatamia vifaranga ni mchakato wa kuwapa vifaranga joto bila kutegemea mama ( joto la balbu au la mkaa) mara baada ya kutotolewa na mashine hadi pale watakapootesha manyoya au watakopoweza kukabiliana na mabadiliko ya ujoto /mazingira .



Mahitaji ya msingi ya kuatamia vifaranga kwa kutumia bruda:
Weka joto la kutosha ili kuwafanya vifaranga wakae starehe (bila usumbufu) wakati wa mchana usiku.
Epuka mabadiliko ya kushtukiza ndani ya banda katika kipindi cha wiki mbili za mwanzo baada ya vifaranga kutotolewa.

MASAA MACHACHE KABLA YA KUINGIZA VIFARANGA;
o    Jaza maji safi kwenye vyombo ili yapate joto kabla ya vifaranga havijaiingia
o   Jaza chakula kwenye vyombo na kudondosha kingine juu ya magazeti
o   Tayari yenye mchanganyiko wa sukari na dawa zinazopendekezwa na watalaam.
o   Hakikisha chumba kina joto la kadri la nyuzi joto 32.5◦c-35◦c.

MAMBO YA KUFANYA WAKATI VIFARANGA VINAFIKA:
1.      Pata idadi yao na kurekodi.
2.      Shika mmoja mmoja na kutumbukiza mdomo wake kwenye maji yaliyowekwa dawa na sukari na chick formula.
3.      Baada ya hapo chunguza tabia ya vifaranga
ili kuona kama joto lilopo ni sahihi au kuna baridi kali au joto kali .
tabia ya vifaranga :
joto likizidi vifaranga wataachama mdomo , kuhema, na kutandaza mabawa. Vilevile hula chakula kidogo na hawachangamki na hukaa mbali na chanzo cha joto(moto)-kigae. Joto likipungua vifaranga hujikusanya pamoja ubavuni mwa kinga ya joto(moto). Hivyo inampasa mhudumiaji kuhakikisha anarekebisha joto katika chanzo kulingana na hali inayojitokeza.


Mambo ya kuzingatia katika kulea vifaranga:
ANGALIA JEDWALI HILI HAPA CHINI.
Umri wa vifaranga [umri katika wiki]
Joto linalofaa
0-1
32.2-35°C(90-95°F)
1-2
29.4-32.2°C(85-90°F)
2-4
26.7-29.4°C(84.3-85°F)

Chakula: Hakikisha vifaranga wanapewa chakula sahihi na kiasi kile kinachopendekezwa kwa umri na uzito hai husika
Mfano.Wape chick marsh vifaranga wa siku moja hadi wanapofikia umri wa mwezi mmoja baada ya hapo watapewa chakula kinachoitwa grower’s marsh/finisher’s marsh. Usikae zaidi ya masaa mawili (2) kabla ya kuwapa kingine.
 usafi:
1.1   Vyombo vya chakula na maji
1.2   Chakula:  Hakikisha chakula safi na maji safi vinapatikana wakati wote. Madini , vitamini na viuatilifu vinawekwa kadri inavyoshauriwa na waganaga wa mifugo.
1.3  Fanya usafi wa kutosha na kuweka dawa kabla ya kuhamishia kuku bandani
1.4    Mazingira ya ndani na nje ya banda ni lazima yawe safi na makavu daima kwani uchafu na unyevunyevu ni chanzo cha vijdudu vya magonjwa kama vile minyoo na kuhara damu.
Epuka usumbufu (stress) mahali wanapoishi vifaranga ,Mfano:
a)      Epuka Kuondoa mfuniko (hoover) wa brooder kila mara.
b)      Kubamiza milango kwa nguvu
c)      Kuruhusu wageni na kuingia kwenye banda bila mpangilio.
d)      Kukaa muda mrefu bila kuwapa chakula
e)      Kuwepo kwa joto jingi katika chanzo.
f)        Utaratibu usiwe wa kubadilika badilika mara kwa mara  mfano chakula  na maji.
g)      Chunguza vifaranga kabla ya kwenda kulala na baada ya kuamka . utaratibu uinaokubalika ni kukesha kwa zamu ili vifaranga wakalaliana na hivyo kusababisha vifo vyo. Kazi ya kulea vifaranga ni ya kujitolea sana hasa katika wiki tano za mwanzo.
1.5  mabanda yawe safi na makavu wakati wote ili kuzuia mazalia na chanzo cha maambukizi kutokana na unyevunyevu.
1.5.Mwanga na mzunguko wa hewa wa kutosha:
Kuna Vianzo viwili vya mwanga navyo ni
1.      Taa ya kandili/kerosene lamp
2.      Taa inayotumia nguvu za umeme- balbu kama vile infrared bulbs.
Mwanga na mzunguko wa hewa ndani ya bruda ni muhimu kwani huvutia na kuvishawishi vifaranga kuanza kula .
Weka madirisha makubwa yenye kuingiza hewa safi na kutoa ile chafu. Banda lisilo na hewa ya kutosha huchochea kuenea kwa magonjwa ya mfumo wa hewa. Andaa nafasi ya kutosha ili kuepuka vifaranga au kuku kurundikana.
v  Chakula bora na cha kutosha:
a)      Wape vifaranga chakula cha kutosha , kizuri na chenye viini lishe vyote .
b)      Wape chakula vifaranfga  kwa vipindi vilivyopangwa badala ya kuwapa mfululizo ili wapate muda wa kutumia chakula walichokula vizuri mwilini.
c)      Hakikisha vyombo vya chakula havikai bila chakula
4.         Madawa:
  Dawa inatakiwa kuwekwa ndani ya chakula na maji ili kuzuia ugonjwa wa kuharisha damu (coccidiosis)
  Dawa ya kideri ni vizuri ikatolewa wakati vifaranga wamefika na au siku chache baada ya kuingizwa kwenye brooder.
  Vitamin huandaliwa wakati mwingine pamoja na madawa kama antibiotics ili zichanganywe kwenye chakula chao.
  Zingatia ratiba ya chanjo inayopendekezwa na wataalamu.
  Kuku wapewe dawa ya kuzuia maumivu ya usumbufu  kwa siku 2-5.
v  Vifaa ndani ya banda la vifaranga:
  Vyombo vya chakula: vyombo vya chakula  vitawekwa sehemu ifaaayo na inayofikika na vifaranga. Hakikisha vifaa havichafuliwi na mavi ya vifaranga au takataka zilizomo ndani ya banda. Hakikisha unaongeza vyombo vya chakula na maji kadri vifaranga wanavyozidi kukua na kuongezeka uzito .
  Vyombo vya maji : – ili kazi ya usafi iwe rahisi umbile na ukubwa wa vyombo vya maji viwe nusu mduara mfano wa muanzi uliopasuliwa katikati. muanzi huu huwekwa katikati ya vijiti viwili vitakavyoushikilia. Vijiti  hivi viwekwe kattika namna ambayo ni rahishi kuvirekebisha. Vilevile kifaa hiki cha maji kinaweza kuwekwa kizibo ambacho kitalegezwa au kuondolewa wakati wa kusafisha. Inashauriwa kuwa vifaa vya kunyweshea viwe na ujazo wa lita tano. Vilevile vifaa hivi viwe vya plastiki ili kuepuka kuotesha kutu.
 Ndoana: hizi ni fimbo za miti au waya ambazo hutmika wakati wa kukamatia kuku kwa ajili ya tiba au kuwauza.
  Toroli au mikokoteni : ikiwa banda limejengwa vizuri , toroli linaweza kusiadia kupunguza idadi ya masaa yatakayotumika wakati wa kulisha au kuweka maji.
 Kuchagua Kundi la vifaranga wenye afya njema:
Chagua  vifaranga wenye afya njema ambayo hutambuliwa kwa kuwa na manyoya makavu, macho maangavu na walio wachangamfu.
Chunguza vifaranga wenye kinyeo kilichochafuka na wazubavu na kisha uwatibu. Vifaranga dhaifu ,wenye vilema na wagonjwa wagonjwa waondolewe katika kundi la kuku (culling).
Vifaranga wa mayai wahamishiwe kwenye banda la kukulia wakiwa na umri wa wiki 6-8 ambako watakaa hadi wiki ya 16-18 kabla ya kuhamishiwa banda la kutagia.
v  Mabadiliko ya hali ya hewa:
Wakati wa majira ya joto kuku hupunguza kula , hivyo wakati huu inashauriwa kumwaga maji juu ya paa la banda ili kupunguza joto.

0 comments:

Post a Comment