Monday, March 6, 2017

CHANJO ZA KUKU - RATIBA MAALUM

Image result for chanjo ya kuku    Image result for chanjo ya kuku

SIKU 1. 
 Baada ya vifaranga kutotoleshwa ndani ya siku moja wapewe glucose kwa muda wa masaa mawili. Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa na baada ya hapo vifaranga wapewe mchanganyiko wa vitamins mfano ni AMINOVIT na OTC plus


Pia hii huchanganywa na maji. Vifaranga wawekwe katika eneo lenye joto wastani na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifaranga wapewe 


2.       SIKU YA 7. 
vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDERI). chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kIsha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye mchanganyiko wa vitamini 


3.     SIKU YA 14. 
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD). Chanjo hii pia huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu, baada ya hapo vifaranga wepewe mchanganyiko wa vitamin. Kuku waliokufa kwa ugonjwa huu unaweza kuwatambua kwa kuchana vifua vyao na hapo utaona vidoti vyekundu kama hapo pichani


4.     Siku ya 21 (wiki ya tatu) 
Rudia chanjo ya Newcastle (Kideri) 


5.     SIKU 28 (Mwezi) 
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD 


6.     SIKU 35 (Mwezi 1 na wiki 1) 
Kipindi hiki kuku wapewe mchanganyiko wa vitamin ya kutosha. 


7.     WIKI YA 6-8 
KUKU wapatiwe kinga ya Ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi kwa mfugaji asiye na utaalam kuwapa kuku, tafuta mtaalum wa mifugo kwa kazi hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.


8.    WIKI YA 8 

Kuku wapatiwe dawa ya minyoo kama Piperazzine na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle

Related Posts:

  • KILIMO CHA NYANYA Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza ku… Read More
  • LISHE YA KUKU NA KUCHANGANYA CHAKULA  LISHE YA KUKU: Ili kuku waweze kuishi, kukua vizuri, kunenepa na kutaga mayai mengi ni lazima wale chakula kingi na chenye ubora unaotakiwa. Uwingi na ubora wa lishe ya kuku unaweza kuainishwa katika makun… Read More
  • KILIMO CHA PILIPILI HOHO Pilipili hoho ni moja ya mazao ya viungo ambayo hulimwa kwa wingi Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Mbeya na Iringa nk. Zao hili hutumika kama kiungo kwenye vyakula mbalimbali kama vile vyama, viazi na ndi… Read More
  • MAGONJWA YA KUKU, DALILI, KINGA NA TIBA Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa… Read More
  • AINA / KOO ZA KUKU KOO ZA KUKU ZINAZOPATIKANA HAPA TANZANIA: Kuna Koo nyingi za kuku wa asili zinazopatikana hapa nchini.                    … Read More

11 comments: