Monday, March 6, 2017

CHANJO ZA KUKU - RATIBA MAALUM

Image result for chanjo ya kuku    Image result for chanjo ya kuku

SIKU 1. 
 Baada ya vifaranga kutotoleshwa ndani ya siku moja wapewe glucose kwa muda wa masaa mawili. Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa na baada ya hapo vifaranga wapewe mchanganyiko wa vitamins mfano ni AMINOVIT na OTC plus


Pia hii huchanganywa na maji. Vifaranga wawekwe katika eneo lenye joto wastani na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifaranga wapewe 


2.       SIKU YA 7. 
vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDERI). chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kIsha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye mchanganyiko wa vitamini 


3.     SIKU YA 14. 
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD). Chanjo hii pia huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu, baada ya hapo vifaranga wepewe mchanganyiko wa vitamin. Kuku waliokufa kwa ugonjwa huu unaweza kuwatambua kwa kuchana vifua vyao na hapo utaona vidoti vyekundu kama hapo pichani


4.     Siku ya 21 (wiki ya tatu) 
Rudia chanjo ya Newcastle (Kideri) 


5.     SIKU 28 (Mwezi) 
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD 


6.     SIKU 35 (Mwezi 1 na wiki 1) 
Kipindi hiki kuku wapewe mchanganyiko wa vitamin ya kutosha. 


7.     WIKI YA 6-8 
KUKU wapatiwe kinga ya Ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi kwa mfugaji asiye na utaalam kuwapa kuku, tafuta mtaalum wa mifugo kwa kazi hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.


8.    WIKI YA 8 

Kuku wapatiwe dawa ya minyoo kama Piperazzine na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle

Related Posts:

  • UFUGAJI BORA WA SUNGURA Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni r… Read More
  • UFUGAJI WA SAMAKI Nyanja ya ufugaji wa samaki inajumuisha ukuzaji wa viumbe vya kwenye maji (bahari na maji baridi) katika mazingira tofauti na yale ya asili. Lengo kuu ni kukuza kwa muda mfupi ili kujipatia lishe, kipato na kutunza mazi… Read More
  • UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA (BROILER). Eneo linalohitajika ni mita mbili (2), Kwa maana ya Urefu wa mita mbili(2) na Upana wa mita moja(1).  Huu ni ufugaji wenye tija kwa wale wafugaji wenye eneo dogo. *Kinakachofanyika katika hilo eneo ni ujenzi wa g… Read More
  • MRADI WA UFUGAJI SUNGURA KIBANDA CHA KUFUGIATunasaidia kwenye ujenzi wa vibanda bora vya sungura,  kwagharama ya Tshs 65,000/=  tu    kwa kimoja cha  ukubwa  wa  futi 2.53  ,  chenye&nb… Read More
  • FURSA MBALIMBALI ZA BIASHARA NA MIRADI Changamkia Fursa mbalimbali ujikwamue Kimaisha Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha. Kutengeneza na kuuza tofali Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmash… Read More

11 comments: