Monday, March 6, 2017

KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO

Image result for KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO

Jina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha. Kilimo hiki kinaendeshwa na wakulima wadogo katika maeneo yenye ukubwa wa kati ya hekta 0.2-0.4 pia kuna maeneo ya wakulima wakubwa wenye hekta kati ya 2-20. Wakulima hao hujishughulisha na kilimo cha zao hilo kwa njia ya mkataba na kampuni hiyo.

Hoho hutumika katika kutengeneza rangi za asili za vyakula ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile zinazotokana na kemikali na pia huongeza ladha na harufu katika vyakula. Hivyo hutumika katika viwanda vya kusindika vyakula, kwa mapishi ya nyumbani na hata katika viwanda vya vipodozi kama rangi ya mdomo, uso n.k. Ina virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kama madini ya chuma, vitamin A na C.
Image result for KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO

2.0 TABIA YA MMEA
Hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene kiasi la duara pia linaweza kuwa lililochongoka,.

3.0 ENEO NA HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO 
Hoho hustawi vema katika maeneo ya usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 2,000 yenye mvua ya wastani wa mm.600-1,250 na wastani wa joto la nyuzi za sentigredi 21 hadi 24. Udongo wa tifitifu wenye rutuba, usiotuamisha maji na wenye hali ya uchachu (pH) kati ya 5.0-6.5 hufaa zaidi. Umwagiliaji ni muhimu pale mvua inapokuwa chache.

4.0 UZALISHAJI
4.1 UTAYARISHAJI WA KITALU

Chagua eneo katika ardhi isiyo na mtelemko mkali na yenye rutuba ya kutosha. Ardhi iwe imepumzishwa bila kuoteshwa mazao ya jamii ya pilipili, biringanya, nyanya, n.k. ili kuepukana na mashambulizi ya wadudu na magonjwa.
Tayarisha kitalu kabla ya msimu wa mvua. Andaa vizuri matuta manne yenye urefu wa wastani wa mita 10 kila moja na upana wa mita moja (1) ili kustawisha miche inayotosha ekari moja.

Acha njia ya nusu mita kati ya tuta na tuta. Mwagilia maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu na endelea kunyweshea kulingana na hali ya hewa na hali ya udongo. Sia mbegu kwenye, mstari, nafasi kati ya mstari na mstari ni sm 10 na kina cha sm1. Kiasi cha mbegu cha nusu kilo kinatosha eneo la hekta moja. Weka matandazo kwenye kitalu au tumia nailoni nyeusi ili kuhifadhi unyevunyevu na kuzuia uotaji wa magugu.

4.2 UTAYARISHAJI WA SHAMBA 

Shamba lilimwe vizuri na kuweka matuta ili kuhifadhi unyevunyevu na kurahisisha umwagiliaji. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.
Image result for KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO

4.3 UPATIKANAJI WA MBEGU

Mbegu ambazo hutumika ni chotara ambazo huuzwa kwenye maduka ya pembejeo za kilimo nchi nzima. Haishauriwi kutumia mbegu kutoka zao la msimu uliopita kwani ubora wa paprika utaharibika na hivyo kuharibu soko unashauriwa kununua mbegu bora.

4.4 UPANDAJI
Mbegu huoteshwa na kukuzwa kitaluni kwa muda wa wiki 6-8 na miche hupandikizwa shambani ikiwa na urefu wa sm.6-10. Mwagilia maji kitaluni kabla ya kuhamisha miche. Panda shambani kwa nafasi ya sm.75-90 kati ya miche kwa sm.90-105 kati ya mistari, wastani wa miche 12,500 itapatikana kwa hekta. Weka samadi shambani tani 25-37 kwa hekta wiki 1-2 kabla ya kupandikiza miche, au kilo 560-670 za NPK (mbolea ya viwandani) kwa hekta kwa uwiano wa 4:7:7 katika udongo usio na rutuba ya kutosha.

ITALIAN PAPRIKA

Image result for KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO italian

5.0 KUHUDUMIA SHAMBA
Palizi ifanyike mara magugu yanapotokea shambani. Umwagiliaji maji ufanyike kama ilivyo kwa mazao mengine kama nyanya. Tumia mbolea kiasi cha kilo 140 za SA au CAN kwa hekta hasa wakati mmea inapotoa matunda ili kupata matunda makubwa na kuvuna kwa muda mrefu (hadi miezi 10).

6.0 MAGONJWA NA WADUDU 


Wadudu 
• Funza wa vitumba
• Vidukari
• Kidomozi (Leaf miner)

Kudhibiti: Tumia dawa aina ya permethrin
Magonjwa
• Kuoza mizizi
• Mnyauko wa majani
• Batobato
Kudhibiti: Choma nyasi kwenye kitalu kabla ya kusia mbegu.
Badilisha mazao yasiyo ya jamii ya pilipili.

7.0 UVUNAJI
Matunda ya kwanza huwa tayari kuvunwa kuanzia miezi 2-3 baada ya kupandikizwa; matunda yaliyokomaa vizuri na kuwa na rangi nyekundu ndiyo huvunwa. Matunda 30-80 hupatikana kwa mmea mmoja.
Ubora wa hoho huongezeka kutegemeana na kiwango cha rangi yake ikiwa ni nyekundu njano au kijani. Mazao kiasi cha tani 3.5 kwa hekta hupatikana. Baada ya kuvuna mwagilia maji, piga dawa (kama ni muhimu) na weka mbolea kuongeza uzalishaji unaofuata.

8.0 USINDIKAJI 

Hoho huuzwa ikiwa bado fresh tofauti na jamii nyingine za pilipili ambazo zinaweza kukaushwa na kusindikwa kasha kuuzwa baadae.

9.0 SOKO LA PAPRIKA 
Soko la hoho lipo nchi nzima kwenya masoko makubwa na hata magengeni, hoho hutumiwa zaidi kama kiungo cha kupikia mapishi mbali mbali au kutia kwenye kachumbari. Tatizo kubwa wanalokabiliana nalo wakulima ni kutokuwa na soko la uhakika ndani na nje ya nchi, mazao huweza kuoza shambani au njiani kutokana na tabu ya usafiri hasa vijijini ambapo mvua zikinyesha barabara hazipitiki kwa urahisi

Kuna aina ya pilipili isiyo kali kama hoho lakini ni ndefu kama pilipili za kawaida ijulikanayo kama PAPRIKA ambayo ina soko kubwa nje ya nchi. Zao hili kwa sasa huzalishwa kwa msukumo wa kampuni ya kigeni ya Hispania inayoitwa Tanzania Spices Ltd iliyopo mkoani Iringa

KILIMO BORA CHA MINAZI

Image result for KILIMO BORA CHA MINAZI


UPANDAJI
Uko wa ina mbili kuna wa vibox na wa pembetatu lakini kwa aina zote mbili umbali wa kupanda ni mita 7.6 kutoka shimo hadi shimo la mnazi, kiasi cha mashimo 175 kwa hecta huingia na kama utatumia mtindo wa pembetatu basi mashimo 13 zaidi yataingia kwa hecta.



Ukubwa wa shimo uwe futi tatu kwa kina, upana na urefu hi kwa maeneo yenye udongo mzuri na wakaida lakini maeneo yenye changarawe, mawe mawe na miamba ukubwa uongezeke hadi futi4 kwa mapana , urefu na kina, Shimo lijazwe majani kiasi cha kilo 15 – 20 unaweza kukisia kama theluthi moja ya shimo au futi moja baada ya kushindilia majani, weka juu yake kama, weka udongo wa juu (top soil) kiasi cha futi moja tena ongezea kiasi cha kilo 10 – 20 cha mbolea ya samadi.

Hakikisha haijai na kufunika shimo lote, pia kama utapata ule udongo mwekundu ambao wengi hupenda kuutumia kwenye bustani zao, pia weka humu kiasi kama utaukosa basi acha vivo hivyo, anza kumwagilia maji wiki moja kabla ya kupanda mbegu yako, kama shimo litatitia ongezea udongo wenye rutuba ya kutosha, kumbuka kuacha kisahani kwa ajili ya kukusanyia maji, ila kama ni sehemu ambazo hufurika kipindi cha mvua jaza udongo hadi kuweka tuta ili maji yasituame.

UPANDAJI
Ni vizuri kutumia mbegu ya nazi moja kwa moja kuliko kutumia miche, hii ni kwa sababu mbili kubwa, kwanza ukinunua mche unakuwa hujui imetoka mnazi gani, wenye ubora gani na hata uzaaji wake huujui, lakini inashauriwa kununua nazi kutoka kwenye mnazi moja kwa moja kwa kuchagua mnazi bora na unaozaa nazi nyingi na kubwa, chagua nazi kubwa zaidi kutoka katika kila mnzi bora.

Nazi ambayo haijafuliwa inakuwa na pembe tatu, moja ya pembe hizi huwa kubwa zaidi na mbili zilizobaki hufanan ukubwa, ule upande mkubwa ulazwe chini wakati wa kupandwa, na upande ule wenye kikonyo ambako nazi hujishika katika matawi ya mnazi (mahanda) ndipo ambapo huota, utatakiwa upatate au upapunguze kwa kisu ili kurahisisha kuota, wakati wa kupanda hakikisha nazi ina maji, ikiwa na maji kidogo sana usiipande, panda miezi miwili au mitatu kabla ya mvua kuanza, nazi inauwezo wa kuota yenyewe bila mvua kwa sababu ina maji ndani yake, ila baada ya kuanza kuota kama hakuna mvua ni muhimu kumwagilia ama sivyo mbegu yako itakufa.

Pia ni muhimu kutumia dawa za kuua mchwa au oil chafu wakati wa kupanda, pia kunadaadhi ya mimea ambayo mizizi yake hufukuza mchwa inaweza kupandwa pamoja na nazi yako. Kama utaamua kutumia miche basi hakikisha miche yako haipungui umri wa miezi sita tangu mbegu kupandwa ili kuzuia miche mingi kufa.

UPANDAJI BORA WA MICHE

Ili kupata mnazi ulio bora mkulima ni lazima awe muangalifu wakati wa kupanda. Mche uliopandwa vibaya huchelewa kukua na hata wakati mwingine hufa. Mazingira kama vile aina ya udongo, kiasi cha mvua, joto, na mwinuko lazima yaangaliwe kwa makini kabla ya kupanda.
Image result for KILIMO BORA CHA MINAZI
MAZINGIRA YANAYOFAA KULIMA MINAZI
Sehemu zinazofaa kulima zao la minazi lazima ziwe na mvua ya kutosha au ziwe na mabonde yenye unyevu ardhini. Kwa kifupi mvua isipungue milimita 1000 hadi 2000 kwa mwaka na kiangazi kisichozidi miezi mitatu.
Sehemu hiyo vilevile iwe na joto la kutosha (23 hadi 30 nyuzi joto) na mwinuko kutoka usawa wa bahari usiozidi mita 600. Minazi inapendelea mwangaza wajua, kwa hivyo isipandwe chini ya miti kama vile miembe au mikorosho.
Image result for KILIMO BORA CHA MINAZI
UCHAGUZI WA ARDHI
Ni vyema kufanya uchaguzi wa ardhLinayofaa kwa minazi kabla ya kupanda.

ARDHI ISIYOFAA KUPANDA MINAZI
Haifai kupanda minazi kwenye ardhi yenye mawe, miamba, jasi na maji yaliyotuama. Sehemu hizi hazifai kwa sababu mizizi ya minazi inapokutana na moja ya hivi, husababisha minazi kudumaa, kubadilika rangi ya makuti kuwa njano badala ya kijani, huacha kuzaa na hatiinaye hufa. Vile vile ardhi yenye kutuanusha maji zaidi ya siku mbili haifai, kwani husababisha mizizi ya minazi kuoza, hivyo kushindwa kupata chakula na mara nyingi niinazi kufa.

ARDHI INAYOFAA KUPANDA MINAZI
Minazi inaweza kustawi katika aina nyingi za udongo, lakini hupendelea zaidi kichanga, tifutifu au kinongo.
Katika seheinu zinazoathiriwa na ukame minazi inaweza kupandwa kwenye maeneo ambayo kina cha maji ardhini wakati wa kiangazi hakizidi mita 3.5 kutoka usawa wa ardhi.

KUTAYARISHA SHAMBA
Baada ya kuchagua sehemu ambayo minazi itapandwa mkulima ni lazima atayarishe shamba mapema kabla ya mvua kuanza. Matayarisho hayo ni pamoja na kufyeka, kung'oa visiki na kuondoa takataka. Kufanya hivi hurahisisha kazi za badaaye hasa upirnaji, palizi na kuzuia wadudu kama vile chonga.

UPIMAJI WA SHAMBA
Upimaji wa shamba ni muhimu kabla ya kupanda miche ya minazi. ·Mkulima anaweza kupima shamba lake kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
(1) Iwapo mkulima anataka kuchanganya mazao mengine kwenye shamba la minazi kama vile michungwa, minanasi, mipera na migomba, inashauriwa kutumia mita 9 kati ya mnazi na mnazi. Mstari hadi mstari mita 15.
(2) Iwapo mknlima atapendelea kupanda minazi peke yake shambani inabidi atumie nafasi ya mita 9x9x9 pembe tatu. Nafasi ya aina hii inafaa kwenye sehemu zenye mvua ya kutosha kama Zanzibar, Tanga, Pangani, bonde la Ng'apa na Mikindani. Sehemu zenye mvua chache kama vile Mtwara, Lindi, Kisarawe, Kibaha na Morogoro inashauriwa kutumia nafasi ya mita 10 kutoka mnazi hadi mnazi na mita 10, kati ya mstari na mstari.
MICHE BORA KWA UPANDAJI
Kabla ya mkulima kupanda miche ya minazi hana budi kuchagua miche iliyo bora. Uwe haukushanibuliwa na wadndu au magonjwa. Uwewenyeafyanamajani yakeyawe kijani. Uwe wenye majani yapatayo sita na uwe nmekaa kitaluni kwa miezi 9.

UCHIMBAJI WA MASHIMO NA UPANDAJI
Ni vizuri mashimo yachimbwe kabla ya mvua'. Kipimo cha kila shimo ni sentimita 60 kwa urefu, upana na kina. Shimo linapochimbwa udongo wajuu utengwe mbali na udongo wa chini. Baadae changanya udongo wa juu na debe moja la samadi au mboji (compost) kama inapatikana. Weka udongo wajuu wenye rutuba zaidi kwanza kwenye shimo, halafu panda mche wako katika shimo. Rudishia udongo wa chini na kuhakikisha kuwa mche wako umeshindiliwa ili usimame barabara.

MAGONJWA YA MINAZI

- KUOZA VIKONYO
Huanza kwa majani machanga mawili ya mwanzo kubadilika rangi na kuwa njano na baadae huwa na vidoti vyeusi hutokea kwenye ukingo, majani hunyauka na kukauka na kisha sehemu ya chini linapoanzia jani huoza na kutoa harufu mbaya ambapo baadae mnazi wote hufa.

Ili kuzuia ugonjwa huu mara tu unapoona dalili za mwanzo tengeneza mchanganyiko ufuatao (gramu 100 za copper sulphate changanya na nusu lita ya maji) + (Gramu 100 za chokaa changanya na nusu lita ya maji) kila moja itengenezwe peke yake halafu kisha vichanganywe pamoja baadae kisha pulizia kwenye minazi iliyoanza kushambuliwa, kama mnazi umeshambuliwa sana ukatwe na kuchomwa moto kuzuia maambukizi zaidi. Pia pulizia mchanganyiko huu msimu wa baridi kuanzi mwezi wa 5 hadi wa 9 kwenye shamba lako kama kinga.

- KUOZA MAJANI
Majani huwa meusi kwenye ukingo na kuti likiliwa zaidi kati kati, majani machanga yakichomoza huwa dhaifu na kisha huchanguka, mnazi haufi ila mazao huwa duni kama ni mnazi unaozaa

ili kuzuia tumia dawa yoyote ya kuzuia fangasi za mimea kama Hexaconazol, Mancozeb au Dithane - M5, muhimu ukufika duka la pembejeo ulizia dawa ya kuua fangasi wa mimea utapata dawa na maelekezo ya kuchanganya usikariri haya majina ya dawa nilizotaja

KILIMO CHA VITUNGUU SAUMU (Garlic)

Image result for KILIMO CHA KITUNGUU SAUMU


UDONGO
Vitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si ya kutosha kwenye udongo, tumia samadi iliyokwisha oza vizuri usitoe samadi bandani na kuipeleka shambani moja kwa moja kwenye shamba la vitunguu thwaumu, labda kama utaliacha shamba bila kulimwa kwa zaidi ya miezi 6, pia unaweza kutumia mbolea za viwandani kama ammonium nitrate, ammonium sulphate, urea n.k wakati wa kupanda na kila baada ya wiki 4 – 6 mara mbili zaidi

UPANDAJI 
Image result for UPANDAJI WA KITUNGUU SAUMU
Kipindi kizuri kwa upandaji ni kipindi ambacho hakuna joto hasa miezi ya May mpaka August kwa Tanzania, Unachukua kitunguu twaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 10 na kati ya mistari ni sentimeta 30. Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kungolewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu thwaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu.
Image result for UPANDAJI WA KITUNGUU SAUMU

UMWAGILIAJI

Kama kuna upungufu wa mvua au ni kipindi cha kiangazi basi ni vizuri ukamwagilia shamba lako, wakati mzuri wa kumwagilia vitunguu twaumu ni asubuhi na sio jioni au mchana, hii inasaidia vitunguu twaumu kujijengea uwezo wa kupambana na magonjwa, baada ya mizi miwili unaweza kupunguza umwagiliajai huku ukiangalia kwa kuchimba kidogo kama vitunguu twaumu vimezaliana vya kutosha na kuanza kukomaa, ukiona vimekomaa acha kabisa kumwagilia ili visioze

UANGALIZI
Aina nyingi za vitunguu twaumu vitakuwa kama vinatoa mbegu kwenye mmea (angalia picha chini), ingawa kuna nadharia nyingi lakini inashauriwa kukata hizi mbegu chini kabisa kwa kisu kikali na kisafi, usikate mapema mara baada ya kutokeza bali subiri mpaka mmea unapoanza kama kujikunja ndipo ukate, kwa wale wanaoacha mbegu hizi ukiamua kuzipanda kwa msimu wa kwanza zitazaa kitunguu kimoja tu cha duara lakini chenyewe ukikipanda tena kwenye mzunguko wa pili kitazaa vitunguu vingi kama kawaida



Ungoleaji wa magugu na majani ni muhimu muda wote ili kuondoa kugombea rutuba, hewa na maji shambani, kwa wenye mashamba makubwa wanaweza kutumia dawa za kemikali kama ROUNDUP na nyinginezo ili kudhibiti magugu, ingawa mimi sishauri hivyo.

MAGONJWA
Magonjwa kama botrytis (kuoza shingo) blue mould na fusarium (kuoza kwa vitunguu) husababisha hasara kubwa kama hayatadhibitiwa kwa kutumia viuatilifu mara unapoona dalili, pia magonjwa kama white rot huchukua zaidi ya miaka 20 kuondoka kama yatavamia shamba lako, inashauriwa kufanya mabadiliko ya zao kila baada ya miaka mitano kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii moja kama vitunguu maji, unaweza kupanda maharage, mahindi, karoti na kabichi katika mzunguko huo. Pia magonjwa kama kutu ya majani husababisha na unyevu mwingi hasa kama mimea itakuwa kwenye udongo unaotuamisha maji au mimea kumwagiliwa jioni au usiku, kumbuka kumwagilia asubuhi tu Ili kudhibiti ugonjwa huu wa kutu mimea ingolewe na ichomwe au utumie viuatilifu vya kuulia fangasi wa mimea.