Monday, March 6, 2017

KILIMO CHA MATIKITI MAJI

Image result for TIKITI MAJI
Ili kulima matikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na ardhi yenye rutuba ya kutosha, matikiti maji hukua haraka kama mimea mimgine ya jamii yake itambaayo mfano Matango, maboga na maskwash.
Kwa mtu ambaye anaanza kilimo yatampa tabu kidogo tofauti na Yule ambaye ana ujuzi kidogo na mambo ya kilimo kwa sababu yanahitaji umakini kiasi.

HALI YA HEWA
Mimea hii haihimili hali ya joto kali sana, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu, inastawi vizuri kwenye kuanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa machi mpaka wa septemba .

UPANDAJI
Panda kwa kutumia Mbegu zinazouzwa madukani, ukitumia Mbegu kutoka kwenye tikiti ulilonunua linaweza likawa ni hybrid na matokeo yake matikiti yatakayozaliwa hayatakuwa bora kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
Panda Mbegu yako moja kwa moja kwenye shamba, usinunue miche au kupanda Mbegu kwenyemifuko ya plastiki halafu ndi uhamishie shambani, panda Mbegu mbili sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 2 - 3 kutoka mstari hadi mstari, baada ya siku chache Mbegu zitaanza kuota, baada ya kama wiki 2 katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi, angalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki.
Unaweza kupandishia udongo kwenye mashina na hii itasaidia kupunguza maji yasituame kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya wa kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda yenye, na wakati wa kuanza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe mimea kwa kuielekezea kwenye waya na kufungia

MCHE ULIOCHIPUA

Image result for MCHE ULIOCHIPUA TIKITI MAJI
UANGALIZI
Miche ikiwa imetambaa kiasi unaweza kuweka matandazo kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu, unaweza kuweka samadi au mbolea za viwandani, mimea ikiwa midogo tumia zaidi mbolea zenye nitrojen na utumie zaidi mbolea za potasiam mara baada ya maua kutokeza hadi matunda kukomaa, matawi yakifikia urefu wa mita 2 kata mbele ilikuruhusu kutoa matawi na hivyo kupata maua mengi zaidi hatimaye mavuno zaidi

MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja, maua dume ambayo ni madogo zadi hutoka kwanza yakifuatiwa na maua jike ambayo ni makubwa zaidi, usipoona maua dume na jike kuna tatizo mfano maji kidogo yalimwagiliwa, upungufu wa viritubisho kwenye udongo, hali ya hewa ni joto/baridi sana n.k
Uchavushaji kwenye matikiti hufanyika na wadudu, kama huwaoni wakifanya kazi yao unaweza kufanya mwenyewe, muda mzuri ni wa asubuhi, unakata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi

UCHAVUSHAJI KWA MKONO


UVUNAJI MATIKITI
Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo, upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu, ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi, hii nayo ni shule nyingine. Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi

MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea, ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kjupata dawa sahii, dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda na FUNGICIDE itasaidia kwa mashambulizi ya fangasi

MAGONJWA MAKUU YA NDEGE

Image result for MAGONJWA MAKUU YA NDEGE

Magonjwa huainishwa kulingana na baiolojia yao,kama Virusi,Bakteria,Kupe,ukungu,na chanzo chao,kwa mfano magonjwa ya lishe yaliyoangaliwa hapo juu.Hata hivyo,magonjwa makuu katika ndege yamegawanywa katika makundi matatu kulingana na makali yao na umuhimu katika mfumo wa uzalishhaji mdogo katika vijiji.Vitu muhimu kama tabia zao wakati wa mlipuko(dalili),na matibabu yanayowezekana(kuzuia ama kudhibiti)vile vile wakati wa kutokea magonjwa hayo.Umuhimu wa ugonjwa huthaminiwa na idadi ya vifo na athari kwa uzalishaji,na itatofautiana kutoka eneo hadi eneo na msimu hadi msimu.

MCHANGANYIKO WA MAGONJWA

Magonjwa kadhaa yasiyo maku yanaweza kukutana na magonjwa mengine na kusababisha madhara makali kwa ndege.Hii ndio hali kwa mfano maambukizo ya E.coli, utapiamlo na kupe wa ndani.Magonjwa kama haya ni vigumu kuua ndege lakini huwa na madhara makubwa kwa kinga ya ndege dhidi ya magonjwa,na kujenga msingi wa maambukizo rahisi ya magonjwa mengine baada ya kuwafanya ndege kuwa dhaifu kiafya.

Umuhimu mkubwa huashiria ugonjwa wa kawaida wenye vifo vingi(zaidi ya asilimia 30 ya kundi),husambaa kwa urahisi na ni vigumu kutibu au hautibiki kabisa.Umuhimu wa wastaani kawaida ,vifo vya wastani(10-30%) kwa kundi na /ama vigumu kutibu.Ugonjwa usio mkuu huashiria wa kawaida, vifo vichache na /ama rahisi kutibu.

UGONJWA WA KUAMBUKIZANA WA KUKU UNAOSHAMBULIA MAPAFU NA MFUMO WA NEVA - NEWCASTLE DISEASE (NCD)
Ugonjwa huu huua, ni wa kawaida katika msimu wa mvua,na hutokea mara kwa mara katika vifaranga wachanga,lakini pia katika kuku waliokomaa.Vifo vya juu katika kundi,mara kwa mara baina ya aslimia 30 na asilimia 80 ya ndege hufa,ugonjwa unapowakumbaKuku hupoteza hamu ya kula na usagaji mbaya wa chakula tumboni.Unaweza kuonyesha upumuaji mzito,kinyesi cha kijani na wakati mwingine kuhara damu. Unaweza kuonyesha dalili za kuchanganyikiwa,kiharusi na hufa ghafla.Dalili zinaweza kutokea zote wakati mmoja.Ugonjwa huu ni wa virusi (virus)kwa hivyo hauna tiba,lakini unaweza kuzuiwa kwa kuwachanja ndege wote ukijumuisha vifaranga wa kutoka wiki mbili.

HOMA YA NDEGE - AVIAN INFLUENZA(AI)

Ugonjwa huu hubebwa na bata na bata maji,na unaweza kusambaa kwa urahisi na ni hatari sana kwa kuku.Vifo vya juu katika kundi,ndevu na panga za jogoo huvimba na kuwa na rangi ya kibuluu (samawati).Husambaa kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa katika madimbwi na vyombo vya maji/chakula.Ugonjwa huu husababishwa na virusi (virus),kwa hivyo hauna tiba.

Ili kujikinga na ugonjwa huu zingatia usafi kwenye banda lako na vyombo vya kuku, ukiona dalili za ugonjwa huu waondoe kuku wagonjwa, wachinjwe na kuchomwa moto. Kabla ya kuingiza kundi lingine la kuku kwenye banda lenye ugonjwa hakikisha unapulizia dawa za kuua virusi ka a VIRU KILL. Mara uonapo dalili za ugonjwa huu muite afisa ugani wa mifugo (Veterinarian)

NDUI YA KUKU - FOWL POX

Huonekana mara kwa mara katika vifaranga wadogo,lakini pia kwenye kuku waliokomaa na huonekana uvimbe mdogo mdogo kwenye ndevu,panga na uso wa kuku.joto la kuku hupanda,uchovu unaoambatana na vifo vya ghafla.Ugonjwa huu ni wa kawaida wakati wa msimu wa kiangazi,lakini pia unaweza kutokea mwaka mzima.Ugonjwa huu ni virusi kwa hivyo hauna tiba.Chanjo inapatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.

UGONJWA WA MAREK - MAREK DISEASE

Huonekana tu katika ndege walio na zaidi ya wiki 16 kwa hiyo hauwapati kuku wa nyama labda kama umewafuga kwa ajili ya uzalishaji (parent stock).Mwanzoni ndege wanaweza kuonyesha bawa moja kushuka au yote mawili.Ama mguu mmoja ama yote inaweza kupooza.Ugonjwa huu ni virusi,kwa hivyo hauna tiba,lakini Chanjo inapatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo

MAAMBUKIZO YA BAKTERIA WA E.coli

Hutokea sana sana katika vifaranga walioanguliwa (Day old chicks),na husababisha maambukizo katika tumbo.Dalili katika ndege wakubwa:kupumua kwa tabu au maambukizo katika mayai na kupungua au kuacha kabisa kwa utagaji kwa kuku wa mayai, kinga bora ni usafi katika mayai kwa ajili ya .Tiba kwa vifaranga wagonjwa inawezekana ukiwa na kiua vijisumu (antibiotics) kama OTC 10%, 20%, 30%.

KIPINDUPINDU CHA KUKU - pasteurellosis

Unaweza kutokea wakati wowote na kwa rika zote.Dalili ni kuharisha sana kwa kuku,kupumua kwa tabu,kukosa hamu ya kula,ndevu na panga za jogoo huwa na rangi ya kibuluu(samawati).Unaweza kutokea kama ugonjwa sugu na kuku kufariki ghafla .Mambukizo kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa.Hauna tiba.kinga ni usafi wa hali ya juu na chanjo.Ua na uchome moto kuku wote walioathirika.Chanjo inapatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.

UGONJWA WA KUHARA VIFARANGA

Ugonjwa huu unasababishwa na bacteria aina ya salmonella pullorum(Bacillary white bacteria)

Hutokea sana sana katika vifaranga wadogo.Vifaranga hutembea kwa tabu sana,tumbo huvimba na hukokota mbawa zao.Kinyesi chao huwa maji maji na hugeuka cheupe.Hauna tiba.Kuzuia ni kutilia usafi maanani.Ikiwa ugonjwa utatokea,tenga ama ua na uchome ndege.Ugonjwa huu husambazwa kwa kifaranga kutoka kwa mayai ya kuku aliyeathirika,ambaye haonyeshi daalili zozote za kuwa mgonjwa.

HOMA YA MATUMBO YA KUKU - TYPHOID

Huonekana zaidi kwenye kuku wakubwa.Dalili:joto huwa kali,uchovu,panga na ndevu za kuku huwa za kibuluu (samawati).Hauna tiba.Kinga ni kutilia usafi maanani na kuua kuku wagonjwa.Usinunue vifaranga kutoka kwenye vyanzo ambavyo hauvijui,na usitumie mayai kwa ajili ya kuanguliwa kutoka kwenye kuku wagonjwa.

GUMBORO - Infectious Bursal Disease(IBD)

Huonekana tu katika vifaranga walio chini ya wiki 6,na ni wa kawaida katika makundi makubwa ambayo yamefugwa katika sehemu zilizofungwa (indoor).Sio wa kawaida katika mfumo mdogo wa ufugaji vijijini.Dalili za kawaida: kuharisha.Ugonjwa huu ni virusi ,kwa hivyo hauna tiba.Chanjo inapatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.

UGONJWA WA KUPUMUA 

Dalili:Pua inayotoka makamasi,uvimbe chini ya macho,macho yaliyojifunga,upungufu katika utagaji wa mayai.Tiba ni kuongeza kiua vijisumu (antibotics) katika maji ya kunywa.

UGONJWA SUGU WA KUPUMUA - Mycoplsmosis

Dalili:Pua inayotoka makamasi ama iliyoziba,uso uliovimba,macho yaliyojifunga,upungufu katika utagaji wa mayai,vifo visivyo vya kawaida.Tiba ni kuongeza kiua vijasumu (antibotics)katika maji ya kunywa.

COCCIDIOSIS 

Ugonjwa huu unaweza kutokea wakati wowote na katika rika zote,lakini unaweza kuzuiwa kwa kusafisha kwa makini nyumba za ndege.Dalili:hali dhoofu ya kuku,kuchoka,kutembea kichwa chini ,manyoya yaliyotimka,kuhara damu.Vifo katika vifaranga wachanga.Ikiwa vifaranga wataendelea kuishi watabakia kuwa wembamba na watachelewa kutaga.Tiba:Weka dawa ya Coccidiostatics katika maji ya kunywa au chakula.Kuzuia:Usiweke ndege wengi pamoja.Epuka kuweka ndege wa rika mbalimbali katika nyumba moja kwani ugonjwa unaweza kusambaa kutoka kwenye kuku wakubwa hadi kwa vifaranga.

MINYOO

Minyoo ni vimelea vya ndani na ni vya kawaida katika umri wote katika mfumo wa uzalishaji vijijini na mjini.Vimelea hivi husababisha afya mbovu,kupoteza uzito,kupungua kwa uzalishaji wa mayai.Tiba bora ni kuongeza dawa ya minyoo kama piperazine katika maji ya kunywa mara moja ama mbili kwa mwaka,ikiwezekana wiki mbili kabla ya chanjo yoyote.

CHAWA, KUPE, VIROBOTO NA UTITIRI

Huvamia rika zote wakati wowote,lakini hutokea mara kwa mara katika nyumba za kuku zenye unyevunyevu na uchafu.Ndege waliokomaa husumbuliwa na hutumia wakati mwingi wakidonoa na kujikuna.Vifaranga wachanga wanaweza kufa kwa sababu ya upungufu wa damu (anaemia).Kama hautatibiwa utitiri,chawa,viroboto,kupe watasababisha kuku kupungua uzito na pia kuna uwezekano wa kupoteza manyoya kwa sababu ya kunyonywa damu na vimelea na kuwashwa na ngozi.Chawa wanaweza kuonekana karibu na macho na pua.Viroboto vinaweza kuonekana kwenye tumbo.Tiba:Nyunyiza dawa ya kuua vimelea kama Akheri powder,jivu na mafuta.Jivu na poda ya salfa inaweza kutumiwa mahali ambapo kuku huoga na mchanga.Viota vinaweza kulindwa kwa kuwekewa majani kadhaa ya tumbaku yaliyochanganywa na jivu katika viota.

MAGAMBA KWENYE MIGUU

Miguu yenye magamba husababishwa na vimelea vya nje vinavyowasha ngozi kwenye miguu ya ndege.Dalili:Miguu ina magamba yanayoonekana na majeraha na anaweza kulemazwa katika kutembea.Tiba:Weka miguu kila siku kwenye mafuta taa,ama katika dawa kuogeshea mifugo hadi magamba yatoweke.

LISHE DUNI

Ndege wanaoathirika zaidi ni wale wanaofugwa ndani kuliko wale wanaojtafutia chakulaDalili:mifupa kukua vibaya na kunyonyoka manyoya.Ndege hutembea kwa tabu;huchopea .Tiba,ukigundua mapema wape ndege wako vitamini na kalsiam ya ziada kwenye chakula, pia wape majani, mabaki ya mboga za majani au kinyesi cha ng'ombe

DONDOO ZA ZIADA KATIKA UFUGAJI WA KUKU

Image result for chanjo ya kuku

VITU AMBAVYO HUTAKIWI KURUHUSU KUKU WAKO WALE.

  • Kuna baadhi ya vitu uwa tunawapa kuku kwa mazoea au tunawaachia tu tunapoona wanakula lakini ukweli vinakuwa na madhara hebu tuviangalie;
  • VITUNGUU
Image result for vitunguu
vitunguu vina sumu iitwayo thiosulphate ambayo huua seli hai nyekundu. Iwapo utalisha kwa kiwango kikubwa itasababisha upungufu wa damu(anaemia) au kifo.
  • MAHARAGWE MABICHI AU YASIYOPIKWA.
Image result for maharagwe
Maharagwe mabichi au yasiyopikwa yana sumu iitwayo hemaglutin ambayo ni hatari kwa kuku kwahiyo unashauriwa kupika au kuchemsha kuondoa sumu hii.
  • MCHELE MKAVU.
Image result for mchele
Kuku wanaolishwa Mchele mkavu kuna hatari mchele huo kujikusanya tumboni na kusababisha matatizo.
  • MAGANDA YA PARACHICHI
Image result for maganda ya parachichi
Kuku wanapokula maganda ya parachichi itapelekea kuingiza sumu mwilini kwa hiyo epuka maganda ya parachichi yasije kujichanganya na chakula.
  • MBEGU ZA APPLE
Image result for MBEGU ZA APPLE
Mbegu za apple zina sumu iitwayo cyanide japokuwa kuku wanapenda apples hakikisha unatoa mbegu.
  • VYAKULA VYENYE CHUMVI NYINGI.
Vyakula vyenye chumvi nyingi husababisha ugonjwa uitwao hypernatremia kwa hiyo mwili wa kuku hauhitaji kiasi kikubwa cha chumvi. Kuku wanaweza kuvumilia kiasi kidogo cha chumvi nacho ni 0.25% kwenye maji. Endapo kutakuwa na uhaba inaweza kupelekea ugonjwa huo.

WADUDU WASUMBUFU KATIKA UFUGAJI WA KUKU ( VIROBOTO, CHAWA NA UTITIRI)
Image result for virobotoImage result for utitiri
Mara nyingi wafugaji wanakabiliwa na changamoto kadhaa katika ufugaji wao wa kuku. Changamoto hizo ni  pamoja na wadudu wasumbufu mbalimbali mfano,  Viroboto, Utitiri na chawa. wadudu hawa wamekuwa tishio kubwa katika kufanya ufugaji wa kuku uwe wenye tija kutokana na kusababisha vifo vingi.

Katika banda lako la kuku ukivamiwa na wadudu hawa kwa hakika afya ya kuku wako itaanza kuzorota kwa haraka na kuwafanya kuku wako waonekane kama wanaumwa vile. Ni wadudu wanaonyonya damu kwa kiasi kikubwa sana na hivyo kusababisha kuku kufa kwa ugonjwa wa kuishiwa damu mwilini. Lakini vilevile kwa kuku wanaotaga huwafanya washushe utagaji wao ghafla. Ukiwatazama unaweza kuona kama wanaumwa kwa maana wanakonda, kuzubaa na kupoteza hamu ya kula. Muda mwingi wanakuwa wanajichokonoa na kujikuna katika manyoya yao kwa kutumia midomo yao. Hii ni kutokana na adha wanayopata hasa kuwashwa na maumivu wanayosababishiwa.

Viroboto ni rahisi kuonekana kwa kuwa wanakaa sehemu za wazi za kuku mfano kuzunguka maeneo ya macho,  katika ndevu na mapanga yao nk. Tatizo ni kwa utitiri na chawa wenyewe si rahisi kuonekana kama mfugaji siyo mfuatiliaji wa karibu wa kuku wake.  Utitiri na chawa wenyewe wanakaa ndani ya manyoya ya kuku kwenye ngozi kabisa. Utitiri ni mdogo kuliko chawa. Chawa wanakuwa weupe hivi wanajishika katika ngozi. Utawaona endapo utapekenyua katika manyoya ya kuku. Wakati utitiri wenyewe unatakiwa uwe na macho mazuri kuweza kuwaona kwa kuwa ni wadudu wadogo zaidi lakini ukipekenyua kwenye  manyoya na kufika ndani kabisa kwenye ngozi utawaona wakitembeatembea. Wanapenda kukaa kwenye kwapa za kuku na kwenye ngozi ya mwili wake

Usipojua vizuri kuhusu wadudu hawa unaweza ukadhani kuwa kuku wako wanaumwa ugonjwa mwingine kabisa katika magonjwa ya kuku. Na kwamba utahangaika kutumia gharama nyingi za madawa huku kuku wako wakiendelea kuzorota bila kupata nafuu ya matibabu unayohatumia. 

Ni muhimu kabla ya kutibu kuku wako ukawasiliana na mtaalamu wa mifugo (Ofisa Ugani) aliye karibu yako ili aweze kukusaidia kukukagulia na kubaini tatizo halisi la kuku wako.  Kwa maana kuku hawahitaji mchezo wa kubahatisha. Unatakiwa ujue ni tatizo gani hasa linawakabili kuku wako ili waweze kupatiwa tiba ya uhakika.

Sasa nini kifanyike kama banda lako litakuwa limevamiwa na Visumbufu hivyo?


Kuna dawa nyingi za kutumia, unaweza kutumia Dawa za unga za kunyunyiza mfano Akheri powder au Sevin (Dudu) Dust. Dawa hizi utanyunyiza kuku wako wote mmoja baada ya mwengine kwenye manyoya yao na sehemu zile ambazo zimevamiwa na wadudu hao mfano machoni na kwenye mapanga yao na vilevile utapaswa dawa hizo kunyunyiza kwenye maranda au vumbivumbi la ndani ya banda la kuku kwa sababu vumbi ni makazi mazuri ya Viroboto na Utitiri.

Lakini wakati mwingine unaweza kujitahidi kutumia dawa hizo za kunyunyiza kwenye mabanda na kuku wenyewe lakini zisifue dafu. Mara nyingi nimeliona hili  kwenye mabanda mengi ya wafugaji. Sasa ukifikia katika hali hii ufumbuzi wa haraka ni kufanya usafi wa banda lako lote. Ondoa maranda na  vumbi lote la samadi kisha deki kwa kutumia dawa ya V- RID Disinfectant. 


Pia utapaswa kupuliza dawa hiyo katika kuta za banda lako. Ukiona tabu kufanya hivyo basi baada ya kuondolewa samadi yote katika banda lako la kuku na kufuta vumbi ukutani, deki kwa maji vizuri bila dawa kisha baada ya banda kukauka vyema paka chokaa kote sakafuni ukutani hadi darini kama banda lako lina dari na kama halina basi utaishia tu katika kuta za banda na sakafuni.

Baada ya kukamilisha zoezi hilo ogesha kuku wako wote kwa kutumia dawa ya Paranex, Tik Tik au dawa yoyote ya kuogeshea mifugoiliyochanganywa kwenye maji yaliyowekwa kwenye dishi kubwa la lita ishirini au arobaini au hata ndoo unaweza kitumia. Uogeshaji utafanyika kwa namna ya kumtumbukiza kuku mmoja mmoja  katika lile dishi au ndoo kisha utamtoa.

Ni tendo linalotumia chini ya nusu dakika. Unamtumbikiza unamtoa unamtumbikiza tena unamtoa ni kama mara mbili hivi lengo ni kuhakikisha kuwa dawa inapenya vizuri katika kila sehemu ya mwili wake.

Baada ya kukamilisha zoezi hilo basi kuku wako watarudi bandani wakiwa wako vizuri na visumbufu vyote vikiwa vimetokomezwa kabisa. Kutokea hapo utaanza kuona sasa afya ya kuku wako ikianza kuimarika na kama walikuwa walishaanza kutaga watarudi katika utagaji wao wa kawaida.

Angalizo. Unapotumia dawa ya kuogesha ni vizuri zoezi hili likafanyika mchana wakati jua linawaka ili kusudi kuku waweze kukingwa na athari ya baridi itakayowasababishia kupata nimonia. Vilevile ni vizuri ukawa na mtaalamu karibu atakayekusaidia kuchanganya dawa kwa uwiano sahihi na maji ili kuepusha madhara kama dawa haitachanganywa katika uwiano